pmbet

Pep amwaga chozi kwasababu ya Klopp

Sisti Herman

May 20, 2024
Share :

Akiwa kwenye mkutano wake na waandishi wa habari mara baada ya kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu Uingereza, Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola jana alimwaga machozi baada ya kuulizwa swali kuhusu kuondoka kwa meneja wa Liverpool, Jurgen Klopp.

"Nitammisi sana, Jurgen amekuwa mtu muhimu sana kwenye maisha yangu ya soka, amenifanya niwe kwenye levo nyingine kwenye maisha yangu.

"Nafikiri tunaheshimiana kila siku na ni mtu wangu wa karibu sana, naona bado anaweza kurudi, nataka kumshukuru sana kwa maneno yake," amesema Guardiola huku akifuta machozi.

Klopp jana aliiongoza Liverpool kwenye mchezo wa mwisho na kuachana na timu hiyo, akiwa anasema kuwa anataka kwenda kupumzika.

Guardiola aliiongoza City kutwaa ubingwa wa sita ndani ya misimu saba jana baada ya timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya West Ham ambapo timu yake ilifikisha pointi 91 mbili mbele ya Arsenal iliyomaliza nafasi ya pili.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet