Perez anataka mechi za UEFA zionyeshwe bure
Sisti Herman
May 18, 2026
Share :

Florentino Pérez anafanya mazungumzo na UEFA ili kufanya soka la Ulaya kuonyeshwa Mubashara bure kabisa. Mpango huo umesukwa na mshauri wake mkuu Anas Laghrari.
Mpango huo wa kimapinduzi unalenga kuondoa usajili wa gharama ya kulipia kwa kila mtazamaji kwa kuzindua jukwaa la wazi la utiririshaji wa kidijitali linalofadhiliwa kabisa na utangazaji jumuishi.
Huku UEFA ikiripotiwa kukaribia kukubali shinikizo hilo ambapo kampuni moja ya vyombo vya habari itatangaza mechi zote za Ligi ya Mabingwa, Ligi ya Europa na Ligi ya Conference moja kwa moja bila malipo, mabadiliko makubwa ambayo yamezua hofu kubwa miongoni mwa makampuni makubwa ya mawasiliano kama vile Telefónica na Orange.





