Perfomance Analysis: Maximo ataja silaha yake ya kuwajua wapinzani
Sisti Herman
September 11, 2025
Share :
Baada ya timu yake kuibuka na ushindi kwenye moja ya mechi zao za michuano ya klabu bingwa ukanda wa nchi za mashariki na kati mwa Afrika (CECAFA), kocha wa klabu ya KMC Marcio Maximo ameweka wazi mchango chanya wa watathmini wa viwango ‘Perfomance Analyst’ kwenye majukumu yake.
“Tunaheshimu kila mchezo, na sasa tutapata tathmini na uchambuzi wa kina kuhusu timu ya Burundi (Vital'O), tuna kundi la watathmini wa viwango vya wapinzani kutoka Degigo Group watakaotupa taswira nzima ya wapinzani, wachezaji wao na kujua mkakati mzuri wa kucheza nao” alisema Maximo baada ya ushindi wa 3-2 dhidi ya Mlandege.
KMC huwatumia wataalamu wa kutathmini na kuchambua viwango vya timu yao na wapinzani kutoka Degigo Sports Management ambao Maximo amekuwa akiwatumia kama silaha ya kuwajua wapinzani wake “nje ndani” kuanzia:
- Uwezo na tabia za kiufundi wa mchezaji mmoja mmoja.
- Takwimu za mchezaji mmoja mmoja ba timu.
- Mbinu za uchezaji za timu (mifumo na staili za uchezaji).
- Ubora na udhaifu wa mchezaji mmoja mmoja na timu.
Baada ya kukusanya taarifa za wapinzani huzichakata na kutengeneza ripoti ambayo huwasilishwa kwa makocha na wachezaji kwaajili ya kutengeneza mpango wa mchezo (Game Plan).
Mchakato mzima wa ukusanyaji wa taarifa hadi uwasilishaji hutumia teknolojia za kisasa ambazo pia timu huzitumia kupima viwango vya ubora wa kiufundi wa wachezaji wake na mbinu za timu mazoezini na kwenye mechi.