pmbet

Pesa si chochote kwenye penzi letu - Mke wa Mane

Sisti Herman

January 16, 2024
Share :

Mke wa mchezaji wa Al Nassr na Senegal, Sadio Mane Aisha Tamba amefunguka kuwa pesa na umaarufu wa mwanaume wake huyo si kitu kwake na hazitombadilisha kwa namna yeyote ile.

 

Aisha mwenye umri wa miaka 18 ameweka wazi hilo kupitia Mail Online "Kwa sasa nipo kwenye maisha mapya najua mambo yatakuwa tofauti lakini sitokuwa na hofu yoyote kwani umaarufu wa Sadio Mane na pesa zake haziwezi kunibalisha jinsi nilivyo". 

 

Aisha ameendelea kwa kusema kuwa "Familia yetu sio watu wa mitandao au kujiachia, nimekulia kwenye mazingira hayo kwa hiyo hakuna kitakachoweza kubadilika baada ya hii ndoa".

 

Sadio Mane na Aisha walifunga Ndoa January 7, 2024 baada ya ndoa hawakukaa na Honey Mood kutokana na msichana huyo kutakiwa kurudi shule kumalizia masomo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet