Piga Ua Man United inatakiwa isimalize msimu ikiwa nje ya 5 bora - Neville
Eric Buyanza
October 20, 2026
Share :

Beki wa zamani na nguli wa Manchester United F.C., Gary Neville, ametoa tahadhari akisisitiza kuwa klabu hiyo lazima imalize ndani ya nafasi tano za juu za msimamo wa Premier League msimu huu wa 2026/27.
Akizungumza kupitia podcast ya Sky Sports, Neville alieleza kuwa kukosa nafasi ya kushiriki michuano ya Champions League msimu ujao kutaitumbukiza klabu hiyo kwenye mdondoko mbaya wa kiuchumi na kimichezo.
"Nafasi ya nne itakuwa ni mafanikio makubwa, ya tano ni kiwango cha kawaida (par), na ya sita ni kufeli," alisema Neville akifafanua malengo ya timu hiyo.
"Lakini hawawezi kumaliza nje ya tano bora, kwa sababu ukikosa Champions League unaingia kwenye mzunguko mbaya. Hautapata wachezaji wakubwa unaowataka kwa sababu wanapenda kucheza Champions League, na utapoteza mapato ya pauni milioni 60 hadi 70. Nafasi ya tano ni lazima kwa Michael Carrick ili kuendeleza ukuaji wa timu."
Neville aliongeza kuwa ingawa bado ni mapema na hakuna haja ya kuwa na hofu kubwa sasa hivi, mambo lazima yabadilike haraka sana katika mechi chache zijazo dhidi ya Bournemouth na Chelsea. Alitahadharisha kuwa kama United itakuwa bado inashikilia nafasi ya 13 hadi kufikia mwezi Januari mwakani, basi Carrick atakuwa kwenye wakati mgumu wa kulinda kibarua chake.





