pmbet

PIGO MANCHESTER CITY: Antoine Semenyo nje ya uwanja kwa wiki nane

Eric Buyanza

October 19, 2026
Share :

Klabu ya Manchester City imepata pigo kubwa baada ya kuthibitishwa kuwa winga wao machachari, Antoine Semenyo, atakuwa nje ya uwanja kwa takriban wiki nane kutokana na jeraha la goti alilolipata mwishoni mwa wiki.

 

Habari hii mbaya imethibitishwa leo, Jumatatu ya tarehe 19 Oktoba 2026, na kocha mkuu wa timu hiyo, Enzo Maresca, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelekea mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA Champions League) dhidi ya AEK Athens.

 

Semenyo, ambaye ni raia wa Ghana, alipata jeraha hilo siku ya Jumamosi, Oktoba 17, 2026, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza (Premier League) ambapo Manchester City waliibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Ipswich Town. Katika mchezo huo, winga huyo aliingia uwanjani akitokea benchi katika dakika ya 77 kabla ya kuumia na kulazimika kufanyiwa vipimo vya dharura.

 

Licha ya habari hiyo ya kusikitisha, kocha Maresca amewatoa hofu mashabiki kwa kueleza kuwa vipimo vilivyofanyika jana Jumapili vimeonyesha kuwa jeraha hilo si baya sana kama ilivyohofiwa mwanzoni.

 

"Habari njema ni kwamba jeraha halihusishi misuli na sio tatizo kubwa sana. Ni tatizo la mshipa wa goti, kwa hiyo tunatarajia atakuwa nje kwa karibu wiki nane," alisema Maresca wakati akitoa taarifa za kitabibu za kikosi chake.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet