pmbet

PIGO ZITO BAYERN: Baba mzazi wa Joshua Kimmich afariki dunia

Eric Buyanza

October 21, 2026
Share :

Klabu ya FC Bayern Munich imepata pigo kubwa kufuatia taarifa za ghafla za kifo cha Berthold Kimmich (57), baba mzazi wa kiungo na nahodha wa timu ya taifa ya Ujerumani, Joshua Kimmich. Vyombo vya habari nchini Ujerumani vimeripoti msiba huo mzito uliotokea leo Oktoba 21, 2026, hatua iliyomfanya nyota huyo kuondolewa kikosini kuelekea mchezo muhimu wa leo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Arsenal ili kupata muda wa kuwa na familia yake.

 

Klabu hiyo imetoa salamu za pole kwa Kimmich na familia yake, huku ikiomba umma na vyombo vya habari kuheshimu faragha yao katika kipindi hiki cha maombolezo. Bayern ilisema inaungana na mchezaji huyo katika wakati huu mgumu, bila kutoa maelezo zaidi kuhusu mazingira ya kifo hicho.

 

Kukosekana kwa Kimmich ni pigo kwa Bayern kuelekea mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa, kutokana na nafasi yake muhimu katika safu ya kiungo. Hata hivyo, kwa sasa jambo la msingi ni kumpa mchezaji huyo na familia yake nafasi ya kuomboleza msiba huo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet