Pipi za pamba 'Kipenzi cha watoto' zinasababisha saratani!
Eric Buyanza
March 4, 2024
Share :
Uchunguzi uliofanywa hivi karibuni na Idara ya Usalama wa Chakula katika jimbo la Tamil Nadu nchini India, umebaini kuwepo kwa kemikali za Rhodamine B katika pipi za pamba ambazo ni kipenzi cha watoto.
Kwa hivyo pipi za pamba za rangi ya waridi na nyekundu, mojawapo ya peremende zinazopendwa zaidi na watoto, sasa zimepigwa marufuku na serikali ya Tamil Nadu.
JE, RHODAMINE B INASABABISHA SARATANI?
Mkuu wa Idara ya Famasia wa Hospitali ya Serikali ya Stanley huko Chennai alisema utumiaji wa Rhodamine B utasababisha uharibifu wa ini.
“Matumizi ya mara kwa mara ya rhodamine B yanaweza pia kusababisha saratani ya ini. Uhusiano kati ya rhodamine B na uharibifu wa ini umethibitishwa katika tafiti nyingi."
Ulaji wa rhodamine B huathiri mfumo wa neva pamoja na ini. Kutokana na hili, kutakuwa na kizuizi katika kazi za ubongo. Dk Chandrasekhar anataja kuwa neva na uharibifu wa uti wa mgongo pia utatokea.
Kwa ujumla, ulaji wa kemikali husababisha madhara makubwa. Haijalishi kemikali hii ni nini, itakuwa na madhara zaidi ikiwa inatumiwa kwa kuendelea.
“Unaweza kusababisha sumu kali mwilini. Hii inaweza kutokea kulingana na kiasi gani cha rhodamine kinachanganywa kwenye chakula na kulingana na mfumo wa kinga wa kila mtu," Dk. Chandrasekhar alieleza alipokuwa akizungumza na Shirika la Habari la Uingereza, BBC.