Pitso apagawa na mido wa Sauzi
Sisti Herman
January 31, 2024
Share :
Kocha wa zamani wa Al Ahly, Mamelod Sundwons na timu ya taifa ya Afrika kusini Pitso Mosimane ameonyesha kukogwa moyo na kiwango cha kiungo wa kati wa timu ya taifa Afrika kusini, Teboho Mokoena kwenye mchezo wa hatua ya 16 bora wakiitoa Morocco kwa mabao 2-0 huku kiungo huyo akifunga kamba 1.
“Teboho Mokoena, mchezaji wa daraja la juu, angalia faulo aliyopiga, nyayo zake zimegusa kila jani la nyasi za uwanja, ametawala eneo la kiungo, habishani na mtu uwanjani” aliandika Pitso kupitia mtandao wake wa kijamii wa X.
Baada ya matokeo hayo sasa Afrika kusini wamefuzu hatua ya robo fainali ambapo watakutana na Cape Verde ambao wanaonekana kuwa tishio kwenye msimu huu wa 33 AFCON.