Pitso ashinda kesi dhidi ya Waarabu, watamlipa Bilioni 3
Sisti Herman
February 26, 2024
Share :
Aliyekuwa kocha wa Mamelod Sundowns, Al Ahly ambaye alitimkia kufundisha Urabuni Pitso Mosimane ameshinda kesi aliyoifungua kwenye mahakama ya usuluhishi wa michezo CAS dhidi ya klabu ya Al Ahli Jeddah ya Saudi Arabia ambayo aliisaidia kupanda daraja kabla hawajaachana naye msimu jana.
Al Ahli watalazimika kumlipa Pitso zaidi ya Rand 22 milioni ambazo ni karibu Bilioni 3 kwa shilingi ya Tanzania.