Pitso atimka Saudia kwa kushindwa kuokoa timu kushuka daraja
Sisti Herman
May 28, 2024
Share :
Wasimamizi wa kocha Pitso Mosimane raia wa Afrika kusini umethibisha kuwa kocha huyo hatoendelea kuwa kocha mkuu wa klabu ya Abha Club ya ligi kuu Saudia baada ya timu kushindwa kubaki ligi kuu nchini humo na mkataba wake kutamatika.
"Nilichagua lazi hii ngumu sana ya kuipokea timu ikiwa mkiani kwenye msimamo wa ligi najua ilikuwa ngumu kubaki lakini nilikuwa na matuamini baada ya kukoka kwenye kushuka daraja mara tatu"
"Sina budi kukubali matokeo yote na mkataba wangu unaisha leo"
Mapema leo uongozi wa kocha huyo MT Sports Management and Agency ulitoa taarifa kwa umma ya kocha huyo kutoendelea kuwa kocha wa timu hiyo.