PLOV: Wali wa Uzbekistan wenye kuongeza 'Nguvu ya tendo' huliwa, Alhamisi tu
Eric Buyanza
April 11, 2024
Share :
Unaitwa Plov, ni mlo wa kitaifa unaopendwa na kuheshimika sana nchini Uzbekistan, unaaminika sana kuwa na uwezo wa kuongeza hamu ya kufanya mapenzi.
Kwa hivyo, kawaida huliwa siku ya Alhamisi pekee, kwa Uzbekistan Alhamisi inachukuliwa kuwa ni siku mahsusi kwa wanawake kupata mimba.
Mlo huu ni mchanganyiko wa mchele, mboga mboga, nyama na viungo, ni maarufu katika nchi zote za ukanda huo, lakini una uhusiano mkubwa na Uzbekistan.
Watu wa Uzbekistan hula plov angalau mara moja kwa wiki.