Pochettino aondoka Chelsea, atajwa United
Sisti Herman
May 22, 2024
Share :
Baada ya klabu ya Chelsea jana kufikia makubaliano ya pande mbili ya kusitisha mkataba na aliyekuwa kocha wao mkuu Mauricio Pochettino kocha huyo ameanza kuhusishwa na timu tofauti ikiwemo Manchester United ambayo inajitafuta upya.
Kocha huyo raia wa Argentina licha ya kutokuwa na msimu mzuri na 'The Blues' lakini mwishoni mwa msimu alionyesha mwanga wa kuendelea kubaki Chelsea kabla maamuzi hayajabadilika.
Akiwa na Chelsea hadi msimu unatamatika Pochettuni alikuwa na;
- Amewaongoza mechi 50
- Wameshinda mechi 27
- Wametoa sare mechi 10
- Wamefungwa mechi 14
Huo ukawa ukarasa wa mwisho wa Pochettino na Chelsea, anaenda wapi? tusubiri tuone!