Pochettino atamani kurejea kuzinoa timu za ligi kuu Uingereza.
Joyce Shedrack
December 6, 2025
Share :
Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Marekani Mauricio Pochettino amekiri kuwa na hamu ya kurejea Ligi Kuu ya Uingereza baada ya "kukaribia sana" kushinda taji akiwa na Tottenham.

Muargentina huyo amekiri kwamba bado anahisi mvuto wa ligi kuu ya Uingereza, hata anapojiandaa kuinoa timu ya taifa ya wanaume ya Marekani kwenye Kombe la Dunia la 2026 katika ardhi ya nyumbani.
Utawala wake kaskazini mwa London uliisha ghafla mnamo Novemba 2019, miezi michache tu baada ya kuiongoza Spurs hadi fainali yao ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa.
Miaka yake mitano na nusu katika klabu ilizaa mechi 293, maendeleo makubwa na kikosi ambacho, kwa muda mfupi, kilionekana kuwa na uwezo wa kufafanua upya historia ya kisasa ya Tottenham.
Alipoulizwa na BBC iwapo anaikumbuka ligi Kuu ya Uingereza,kocha huyo mwenye umri wa miaka 52 alisema: "Ndio, mimi hutazama sana. Ligi ya Uingereza ndiyo bora zaidi duniani. Bila shaka, ninaikosa. Nina furaha sana Marekani, lakini huwa nafikiria kurejea siku moja. Ni ligi yenye ushindani zaidi, na bila shaka, ningependa kurejea tena."





