Pogba adata na 'Komasava' ya Diamond
Sisti Herman
May 24, 2024
Share :
Aliyekuwa mchezaji wa Manchester United, Juventus na Ufaransa Paul Pogba na familia yake kupitia kurasa zao za Instagram wameonekana kucheza challenge ya wimbo wa msanii wa kimataifa wa Tanzania Diamond Platnumz 'Komasava' #komasavachallenge!
Ngoma hiyo iliyoimbwa kwa lugha mbalimbali imeendelea kukata mawimbi kwa kufika na kuchezwa maeneo mbalimbali duniani kupitia 'platform' tofauti.
Hadi sasa ngoma hiyo ina watazamaji ina watazamaji milioni 1.3 kwenye mtandao wa Youtube ikiwa na wiki tatu tu huku ikiendelea kutamba kwenye majukwaa mbalimbali ya kutazama na kusikiliza muziki.