Pogba; Sijastaafu soka, bado napambana nirudi
Sisti Herman
July 2, 2024
Share :
Aliyekuwa kiungo wa kati wa kalbu ya Manchester United, Juventus na timu ya Taifa ya Ufaransa Paul Pogba ambaye amefungiwa kucheza soka kwa miaka minne kwa matumizi ya dawa zisizoruhusiwa michezoni amesema bado hajastaafu kucheza soka bali anaendelea kupambana ili aweze kurejea uwanjani.
"Bado sijastaafu kucheza soka, bado napambania maisha yangu ya soka, nafanya mazoezi sana bado sijaisha" alisema Pogba alipoulizwa kuhusu maisha yake ya soka baada ya kumaliza kifungo.
Pogba ameyasema hayo kupitia kituo cha habari za michezo cha Sky Sports jana alipohudhuria mchezo wa mtoano wa hatua ya 16 bora kati ya Ufaransa na Ubelgiji, Ufaransa wakishinda 1-0.