Poland yapunguza kodi kwa wazazi wenye watoto wawili.
Joyce Shedrack
November 17, 2025
Share :
Serikali ya Poland imetangaza sheria mpya inayopunguza mzigo wa kodi kwa wazazi walio na watoto wawili au zaidi, ikiwa ni hatua ya

kuimarisha ustawi wa familia na kuongeza kipato kinachobaki mikononi mwa wazazi. Kwa mujibu wa tangazo hilo, wazazi wenye watoto wawili au zaidi hawatalipa kodi ya mapato.
Sheria hii inawagusa wazazi wa kawaida, Lengo kuu ikiwa ni kupunguza gharama za maisha, kuongeza motisha ya kulea watoto, na kuchochea viwango vya uzazi ambavyo vimekuwa vikishuka nchini humo.
Serikali ya Poland inaamini hatua hii itaimarisha uwezo wa kifedha wa familia na kusaidia kujenga nguvu kazi imara kwa vizazi vijavyo.





