Polisi auza Uniform yake mtumbani kwa Elfu 12
Eric Buyanza
February 7, 2024
Share :
Inspekta wa polisi aliyeuza mtandaoni suruali yake ya kazi kwa pauni 4 (shilingi elfu 12) amepewa adhabu ya kushushwa cheo.
Owen Hurley wa kituo cha Polisi cha Hertfordshire na ambaye amehudumu kwenye kazi hiyo kwa miaka 15, alikiri kuwa aliuza uniform hiyo mtandaoni kama mtumba, kwani ilikuwa imechakaa na pili alikuwa na nia kupunguza vitu kwenye kabati lake la nguo lililokuwa limejaa.