pmbet

Polisi wamsaka dereva wa gari taka aliyewagonga wanne Moro

Sisti Herman

September 29, 2024
Share :

Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linamtafuta dereva wa gari la kubeba Taka lenye namba za usajili T 882 DQJ aina ya Isuzu Tiper. Dereva wa gari hilo alishindwa kudhibiti gari hilo alilokuwa analiendesha na kusababisha kuwagonga watu wanne ambapo wawili kati yao wamefariki na wawili wamelazwa hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Morogoro. 

Taarifa ya Polisi kwa umma inaeleza kuwa gari hilo liligonga bajaji MC 445 DRG iloyokuwa inasubiri abiria. Ajali hiyo imetokea Septemba 28,2024 jioni eneo la makutano ya barabara Morogoro Dodoma na barabara ya Kihonda Maghorofani baada ya dereva anayetafutwa kushindwa kulimudu gari lake na kuwagonga wafanyabiashara wanaopanga biashara zao kando kando ya Barabara. 

Waliofariki dunia wamefahamika kuwa ni 1. Lisa Zakaria Josia (20) 2. Habibu Shabani Nassoro (63). Majeruhi ni 1. Paul Vitalis Temba (71) na 2. Josephiner Francis Mbago (48). 

Uchunguzi wa awali umebaini chanzo cha ajali ni kuharibika kwa mifumo ya breki ya gari hilo la kubeba taka hivyo kusababisha dereva kushindwa kulimudu gari lake. 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet