pmbet

Polisi wanachunguza kifo mchezaji wa bafana Jayden Adams

Eric Buyanza

July 13, 2026
Share :

Polisi nchini Afrika Kusini wameanzisha uchunguzi kuhusu kifo cha mchezaji wa timu ya taifa, Jayden Adams, baada ya mwili wake kupatikana katika nyumba moja jijini Cape Town mwishoni mwa wiki.

 

Adams, aliyekuwa na umri wa miaka 25, alifariki dunia wiki mbili tu baada ya kuisaidia timu ya taifa ya Afrika Kusini kufuzu hatua ya mtoano ya Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza katika historia yake.

 

Hadi sasa, mamlaka hazijatangaza chanzo cha kifo chake.
 

Katika taarifa iliyotumwa kwa shirika la habari la Associated Press (AP), polisi walisema kuwa kituo cha polisi cha Cape Town Central kilifungua jalada la uchunguzi baada ya mwili wa mwanaume mwenye umri wa miaka 25 kupatikana siku ya Jumamosi.

 

Kwa mujibu wa polisi, mwili huo ulipatikana majira ya saa 5:00 asubuhi kwa saa za nchini humo katika nyumba iliyopo eneo la Schotsche Kloof, jijini Cape Town, ingawa hawakutoa taarifa zaidi kuhusu mazingira ya tukio hilo.
 

Baba wa marehemu, Juanito Adams, aliliambia shirika la habari la televisheni la eNCA siku ya Jumapili kuwa familia bado inasubiri matokeo ya uchunguzi wa maiti (postmortem) ili kubaini chanzo cha kifo, na kwamba hadi sasa hawajapanga tarehe ya mazishi.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet