pmbet

Polisi wapekua makazi ya Rais, atuhumiwa kujimilikisha mali na saa za kitajiri

Eric Buyanza

April 3, 2024
Share :

Rais wa kwanza mwanamke wa Peru, Dina Boluarte anachunguzwa kwa kujitajirisha kinyume cha sheria.
 

Dina Boluarte, amekumbwa na kashfa ya kumiliki mkusanyiko wa saa za Rolex na vito vya kifahari ambavyo vimemuweka katikati ya uchunguzi wa ufisadi.
 

Wiki iliyopita, polisi walivamia makazi yake binafsi na ikulu kwa ukaguzi wa mali ambazo zimekuwa zikitiliwa mashaka ya jinsi alivyozipata.
 

Hata hivyo Rais huyo amekiri kumiliki saa moja aina ya Rolex na vitu vito vyenye thamani kubwa lakini akashindwa kueleza namna alivyopata vitu hivyo licha ya kupata mshahara wa $3,320 kwa mwezi (sawa na shilingi milioni 8.5 za kibongo).
 

Mwenyewe Rais Boluarte amekuwa akikanusha tuhuma za kujitajirisha kinyume cha sheria.
 

Kumekuwa na shinikizo la kutaka rais huyo aondolewe madarakani, kutokana na matatizo yaliyoenea nchi nzima, ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa vitendo vya uhalifu.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet