Polisi waua wakisaidia mauaji yasitokee
Sisti Herman
December 31, 2023
Share :
Polisi huko Los Angeles, nchini Marekani wameachia video inayoonyesha mwanamke aliyejulikana kwa jina la Niani Finlayson, mwenye umri wa miaka 27, akipigwa risasi na moja ya Maafisa wa Polisi, waliofika nyumbani kwa Finlayson, baada ya mwanamke huyo kutoa taarifa ya kunyanyaswa na mpenzi wake.
Idara hiyo imesema, Finlayson alipiga simu ya msaada ya 911, akiomba usaidizi wa kumuondoa mpenzi wake ambaye hataki kumuacha, ambapo kupitia sauti iliyorekodiwa na idara ya msaada, alisikika akipiga kelele za kumtaka mtu aondoe mikono yake, kutoka kwenye mwili wake.
Tracie Hall, ambaye ni mama wa Finlayson, amesema alielezwa na binti wa Finlayson mwenye umri wa miaka 9 kuwa, mwanaume huyo alimkaba mama yake, na hata binti huyo alipojaribu kumsaidia mama yake alisukumwa na mwanaume huyo.
Kulingana na video hiyo, ilionyesha Maafisa watatu wakifika kwenye makazi ya Finlayson, ambapo alionekana ameshika kisu akitishia kumchoma mwanaume huyo ndipo Afisa wa Polisi alipomfyatulia risasi nne mwanamke huyo.