Polisi yaanika majina ya watu waliokamatwa kwenye maandamano.
Joyce Shedrack
September 23, 2024
Share :
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limetoa orodha ya majina ya watu 14 waliokamatwa na jeshi hilo baada ya kwenda kinyume na katazo walilotoa kuhusu maandamano yaliyoandaliwa na Chadema.
Kupitia taarifa iliyotolewa leo muda mchache uliopita imebainisha majina ya watu wanaoshikiliwa kwa ajili ya mahojiano miongoni mwao wakiwemo Viongozi wakubwa wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema.
Taarifa hiyo imesema "Viongozi wa chama hicho walipanga kufanya maandamano tarehe 23/09/2024 ambayo Jeshi la Polisi lilitoa katazo la kutofanyika na kuyapiga marufuku. Aidha tarehe 23/09/2024 baadhi ya watu waliokwenda kinyume na katazo hilo la maandamano yaliyopigwa marufuku wamekamatwa na kuhojiwa kama ifuatavyo.
1. FREEMAN AIKAEL MBOWE
2. TUNDU ANTIPAS LISSU
3 . GODBLESS LEMA.
4. PETER LAZARO NGOLONGI
5. SHEIKH OMARY FAKHI
6. REVOCATUS THEODORY MLAY.
7. PAULO SHIJASON MUSISI
8. SHABAN MABELA KINDE
9. ABUBAKARI ABEID MUGALU.
10. EMMANUEL REUBEN NTOBI
11. SYLIVESTER GASPER SATU.
12. RACHEL PETER MLONDELA
13. MARY ISACK NUNGI
14. BAKARI HABIBU SALUM
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linatoa wito kwa wananchi wote kutojihusisha wala kujiingiza katika makundi ya uhalifu kwani kufanya hivyo watakuwa wanafanya makosa ya jinai na wakikamatwa watachulikuliwa hatua za kisheria". Imesema taarifa iliyotelewa na Jeshi la Polisi.





