Polisi yathibisha kuwakamata Diva The Bawse na Niffer.
Joyce Shedrack
November 19, 2024
Share :
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limethibitisha kumkamata mtangazaji wa Wasafi Diva Gissele Malinzi maarufu Diva The bawse pamoja na Mfanyabiashara Jenifer Jovin maarufu Niffer kwa tuhuma za kukusanya fedha za maafa ya kariakoo bila kibali.

Kupitia taarifa iliyotolewa leo na Jeshi la Polisi imeeleza kuwa imemkamata Diva mkazi wa Mikocheni pamoja na Niffer Mkazi wa Salasala Kinondoni ambaye amekamatwa Dodoma na kurejeshwa Dar es Salaam kwa ajili ya mahojiano zaidi.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema litashirikiana na mamlaka zingine za kisheria kuona hatua zaidi zinazopaswa kuchukuliwa dhidi ya watuhumiwa hao wawili.





