pmbet

Polisi yawanasa wezi 4 wa magari - Muliro

Eric Buyanza

May 24, 2024
Share :

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limewakamata watu wanne kwa tuhuma za wizi wa magari 12 na na bajaji tano katika maeneo mbalimbali jijini Dar es salaam.

Kamanda wa Polisi kanda Hiyo, Jumanne Muliro amesema hiyo inatokana na operesheni maalum iliyoanza Desemba 2023 hadi Mei 22, mwaka huu na kwamba tayari wahusika wameshatambua magari yao.

“Watuhumiwa hao walikuwa wakiyaiba magari hayo, kufuta namba za usajili wa gari (Chasis) na kubadilisha plate namba halafu kuyauza tena yakiwa na kadi za bandia,” amesema Kamanda Muliro na kuwataja watuhumiwa hao ni Haruni Selemani (34) mkazi wa Yombo Makangarawe, Temeke na wenzake watatu.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet