pmbet

Polisi yawasaka 'Wasuka Dread' ikiwahusisha na uhalifu

Eric Buyanza

December 18, 2023
Share :

Huko Sudan ya kusini hali ni tete baada ya polisi kupitisha msako wa kuwasaka wahalifu, huku watu wenye 'Dreadlocks' wakiwa miongoni mwao.
 

Tangu mwezi November mpaka sasa, polisi jijini Juba wameshawakamata mamia ya vijana wenye dreadlocks wakiwatuhumu kwa uhalifu...baadhi ya waliokamatwa wako wasanii na watu wengine maarufu.
 

Katika kisa cha karibuni wasanii wawili maarufu nchini humo walilazimishwa kunyoa dreadlocks ndani ya kituo polisi kabla ya kuachiwa huru.
 

Kamatakamata hiyo imeleta sintofahamu nchini humo, huko watetezi wa haki za kibinadamu wakisema polisi wanaingilia uhuru binafsi wa wananchi.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet