Poshy Queen afunguka chanzo cha ugomvi wake na Harmonize.
Joyce Shedrack
August 17, 2024
Share :
Mrembo na mfanyabiashara Poshqueen amefunguka kuhusiana na ugomvi wake yeye na mpenzi wake wa sasa mwanamuziki Harmonize uliotokea siku chache zilizopita na kusisistiza hawakugombana siku ya sherehe ya yanga.
“Mimi na Harmonize hatukugombana kisa kauli aliyotoa kuhusu wanawake wa Yanga lakini pia hatukugombana katika tafrija baada ya siku ya Yanga, ugomvi wetu niwamambo yakimahusiano na sichochote kile, lakini pia yanayosemwa sio yakweli” amesema Posh
Wawili hao walianza mahusiano Januari 2024 ambapo mpaka kufikia sasa wametimiza miezi nane kwenye uhusiano huo ambao mara kadhaa wamekuwa na mtafaruko ambao umekuwa ukisababisha kila mmoja kufuta picha za mwenzake kwenye mitandao yao ya kijamii.





