Precious wa Yanga Princess atambulishwa Simba Queens
Sisti Herman
July 30, 2024
Share :
Baada ya jana kunasa saini ya Amina Ally Bilal kutoka JKT Queens, Klabu ya Simba Queens leo imemtambulisha rasmi kiungo mshambuliaji wa Nigeria Precious Christopher kuwa mchezaji wao kutokea Yanga Princess.
Kama tulivyochspisha wiki iliyopita kuwa Simba Queens imekamilisha uhamisho wa wachezaji watatu wa kimataifa kutoka Yanga, Precious ametangulia kutambulishwa huku Utambulisho wa wengine wawili ukifuatia ambao ni;
- Wincate Kaari, beki wa kushoto wa timu ya Taifa ya Kenya
- Marry Saiki Atunike, kiungo wa kimataifa wa Nigeria