pmbet

Presha ya kazi Newcastle, yamkimbiza Eddie Howe

Eric Buyanza

July 30, 2026
Share :

Kocha Eddie Howe ameondoka rasmi Newcastle United kwa makubaliano ya pamoja na uongozi wa klabu hiyo. Taarifa hizi zimeshathibitishwa na vyombo vikubwa vya habari kama Sky Sports na BBC Sport.

 

Howe ameuambia uongozi wa klabu kuwa anajisikia kuchoka sana kiakili na kimwili kutokana na presha ya kazi, hivyo anahitaji kupumzika kwanza kwenye masuala ya soka.

 

Amekuwa na manung'uniko kuhusu mwelekeo wa timu kwenye soko la usajili. Newcastle imelazimika kuuza wachezaji wake tegemeo kama Anthony Gordon kwenda Barcelona na Sandro Tonali.

 

Newcastle ilimaliza katika nafasi ya 12 kwenye msimu wa Ligi Kuu ya Uingereza (Premier League) uliopita, hali iliyoongeza shinikizo na ukosoaji mkubwa kutoka kwa mashabiki.


Kocha wa Kijerumani, Matthias Jaissle, ambaye kwa sasa anafundisha klabu ya Al Ahli ya Saudi Arabia anatarajiwa kubeba mikoba.
Taarifa zinasema mazungumzo kati ya uongozi wa Newcastle na Matthias yapo kwenye hatua za mwisho.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet