Private Jet yapata ajali na kuua watu 9 Florida
Sisti Herman
November 2, 2026
Share :

Mawasiliano ya mwisho ya redio yenye kutisha yamebainika kufuatia ajali ya ndege binafsi iliyoanguka katika eneo la makazi huko Florida, na kusababisha vifo vya watu wote tisa waliokuwemo ndani.
Ndege hiyo aina ya Learjet 60 ilikuwa ikitoka Austin, Texas, kuelekea Bahamas wakati ghafla ilipoanza kudondoka kuelekea ardhini. Rubani alitoa wito wa dharura wa "Mayday," akiripoti kuwa ndege hiyo ilikuwa ikishuka kwa kasi ya futi 20,000 kwa dakika.
Muda mfupi kabla ya kuanguka, sauti ya mtu kutoka ndani ya chumba cha rubani ilisikika ikipiga kelele: "Hatuna muda tena!"
Ndege hiyo ilianguka kwa kishindo katika eneo la Palm Beach County na kushika moto mkubwa. Mamlaka za shirikisho zinafanya uchunguzi kubaini chanzo cha ajali hiyo.





