Prof. Janabi; Tujenge viwanda vyetu ili tupunguze gharama
Sisti Herman
June 5, 2025
Share :
Mkurugenzi wa Shirika la Afya duniani kanda ya Afrika Prof. Mohammed Janabi amesema kuwa moja kati ya mambo atakayosimamia ni kuhakikisha kuwa bara la Afrika linakuwa na viwanda vingi vya dawa za binadamu ili kupunguza Gharama za kuagiza madawa kutoka nje ya bara.
"Nitasimamia sana kupitia mawaziri wetu wa afya na serikali zao kwamba tuanze na viwanda vyetu. Tukiwa na viwanda vyetu [Afrika] tutaweza kununua dawa humu humu wenyewe kwa wenyewe, dawa zitakuwa zimeshuka. Lakini hii kwamba kila siku dawa zitoke nje, vitenganishi vitoke nje, chanzo zitoke nje, utapewa dawa hizo kwa uwezo wako." alisema Profesa Mohamed Janabi, Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika