pmbet

PSG iko tayari kuvunja mkataba wa Osimhen

Eric Buyanza

February 13, 2024
Share :

Paris Saint-Germain iko tayari kutoa euro milioni 120 kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa Napoli, Victor Osimhen kwenye msimu wa majira ya joto.

Kulingana na vyanzo kadhaa, dau la kuvunja mkataba mpya wa Osimhen aliosaini na Napoli mwaka jana ni takriban euro milioni 120 mpaka 130. 

Inaripotiwa kuwa PSG watakuwa tayari kuwasilisha ofa rasmi kwa Osimhen mwishoni mwa msimu huu.

PSG wanamuona Osimhen kama mbadala mzuri wa Kylian Mbappe, ambaye anaweza kuhamia Real Madrid.

Osimhen amefunga mabao nane katika mechi 18 alizoichezea Napoli msimu huu.

Anatarajiwa kurejea Napoli wiki hii baada ya kushiriki Kombe la Mataifa ya Afrika 2023 lililotamatika mwishoni mwa wiki.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet