PSG imestahili kukutana na Arsenal - Steven Gerrard
Eric Buyanza
May 7, 2026
Share :
Gwiji wa Liverpool, Steven Gerrard, ameitaja Paris Saint-Germain kuwa klabu ambayo ilistahili kukutana na Arsenal katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Kiungo huyo wa zamani wa England alisema hayo mara baada ya PSG kuiondoa Bayern Munich katika hatua ya 4 bora ya Ligi ya Mabingwa.
Usiku wa jana Jumatano PSG ilitoka sare ya 1-1 dhidi ya vijana wa Vincent Kompany kwenye Uwanja wa Allianz Arena na kufuzu kwa fainali ya Ligi ya Mabingwa, shukrani kwa ushindi wa jumla wa 6-5.
"Bayern Munich wamelazimisha sare, lakini timu bora imepita” alisema Steven Gerrard.






