pmbet

PSG Kumsajili kaka yake Desire Doue,Guela Doue kuwa mbadala wa Hakimi.

Joyce Shedrack

June 26, 2026
Share :

Klabu ya PSG inampango wa kumsajili beki wa kulia Guela Doue ambaye ni ndugu wa damu wa nyota wao Desire Doue ambaye atakuwa mbadala wa kuaminika wa nyota wao, Achraf Hakimi, baada ya kushindwa kupata mchezaji wa nafasi hiyo msimu uliopita.

Strasbourg-PSG : Quand Désiré Doué provoque son frère Guéla

Baada ya kushindwa kabisa kumsajili beki wa kulia msimu uliopita, mkurugenzi wa michezo wa PSG, Luis Campos, ameanza upya juhudi za kumtafuta mchezaji wa asili wa nafasi hiyo kutokana na msimu uliopita kulazimika kutumia viungo Warren Zaïre-Emery na João Neves kucheza nafasi ya beki wa kulia wakati Hakimi alipokosekana.

 

PSG wameelekeza macho yao kwa Guela Doué mwenye umri wa miaka 23, ambaye alikuwa na msimu bora akiitumikia klabu yake ya Strasbourg baada ya kusaini mkataba unaomuweka klabuni hapo hadi Juni 2029.

 

Umaarufu wa Guela umeongezeka zaidi kutokana na kiwango chake kizuri akiwa na timu ya taifa ya Ivory Coast kwenye Kombe la Dunia la 2026, ambapo alicheza mechi tatu na kusaidia timu yake kufuzu hatua ya mtoano ya timu 32. Alianza katika ushindi dhidi ya Ecuador na Curaçao, kisha akaingia kama mchezaji wa akiba mwishoni mwa mchezo dhidi ya Germany, jambo lililovutia vilabu vikubwa kama Borussia Dortmund.

 

 

 

 

 

 

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet