pmbet

PSG watachukua ubingwa, ni ngumu kuwashinda - Steven Gerrard

Eric Buyanza

April 30, 2026
Share :

Gwiji wa Liverpool, Steven Gerrard, ameitabiria klabu ya PSG kuwa ndiyo timu itakayoshinda ubingwa wa Ligi ya Mabingwa msimu huu.

 

Akiongea kwenye TNT Sports, Gerrard alisema kwamba mabingwa hao a Ligue 1 ya Ufaransa ni ngumu kuwashinda.

 

Haya yanajiri baada ya PSG kuishinda Bayern Munich 5-4 katika mechi ya mkondo wa kwanza wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa siku ya Jumanne.
Alipoulizwa ni timu gani ataweka pesa zake kushinda Ligi ya Mabingwa, Gerrard alisema, "Imekuwa PSG tangu mwanzo.

 

"Sijaweka dau la fedha, lakini chaguo langu ni PSG. Nadhani ni wazuri sana wanapokuwa kwenye ubora wao, ni wagumu sana kuwashinda."

PSG itahitaji kuonyesha kiwango bora dhidi ya Bayern Munich kwenye Uwanja wa Allianz Arena wiki ijayo ili kuweza kutinga fainali ya Ligi ya Mabingwa.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet