PSG watuma ofa nzito kwa Sancho
Sisti Herman
July 23, 2024
Share :
Klabu ya Paris Saint-Germain (PSG) ya Ufaransa imetuma ofa ya kuhitaji saini ya mshambuliaji wa klabu ya Manchester United Jadon Sancho ambaye tayari amerejea kwenye klabu yake wakati huu wa maandalizi ya msimu.
Sancho ambaye alikuwa na kiwango bora ngwe ya pili ya msimu uliomalizika akiwa na Borrussia Dortmund iliyofika fainali ya ligi ya Mabingwa Ulaya alicheza michezo 21 akifunga mabao matatu na kutoa pasi za magoli 2 kwenye ligi kuu Ujerumani na ligi ya Mabingwa Ulaya.
Uwezekano wa Sancho kuendelea kubaki United haupo kwa asilimia zote kutokana na mahusiano baina ya Mchezaji, Kocha na klabu kutokana na mapungufu ya kinidhamu aliyowahi kuonyesha Sancho msimu jana.