PSG yavunja Benki, yatoa ofa ya Euro milioni 250 kumsajili kinda Yamal
Eric Buyanza
June 29, 2024
Share :
Klabu ya Paris Saint-Germain ya Ufaransa inaripotiwa kuwa tayari kuvunja benki ili kumsajili mshambuliaji kinda wa Barcelona, Lamine Yamal.
Mabingwa hao wa Ligue 1, wamekuwa wakimtanani kinda huyo mwenye kipaji cha hali ya juu kwa muda mrefu, na walishaweka mezani ofa yao ya kitita cha euro milioni 200 ili kuinasa saini yake, lakini Barcelona walichomoa kwasababu hawakuwa na mpango wa kuachana na mchezaji huyo.
Sasa Mundo Deportivo wanaripoti kuwa, PSG wameongeza ofa yao na sasa wako tayari kutoa euro milioni 250 kwa ajili ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania.