PSG yawapora Man Ut Mido wa Ureno sokoni
Sisti Herman
July 30, 2024
Share :
Klabu ya PSG ya ligi kuu nchini Ufaransa ipo kwenye hatua za mwisho kukamilisha usajili wa kiungo wa kati kinda wa timu ya Taifa Ureno Joao Neves kutoka klabu ya Benfica ya Ureno.
Kinda huyo mwenye umri wa miaka 19 ambaye pia aliwaniwa vikali na klabu ya Manchester United anaweza kujiunga na PSG masaa machache yajayo kwa ada ya uhamisho ya Paundi milioni 70 (zaidi ya Tsh Bilioni 243).