PSG yazuiwa kuvaa jezi yake yenye nyota mbili
Eric Buyanza
August 12, 2026
Share :

Klabu ya Paris Saint-Germain (PSG) ya Ufaransa imekatazwa kuvaa jezi zenye nyota mbili kwenye mechi za Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1) kwa sababu kanuni za ligi hiyo haziruhusu mabadiliko ya nembo za vilabu katikati ya msimu.
PSG waliongeza nyota hizo mbili juu ya nembo yao wakati wa mechi za kirafiki za maandalizi ya msimu (pre-season). Nyota hizo ziliwekwa kusherehekea ubingwa wao wa back-to-back wa mashindano ya UEFA Champions League (2025 na 2026).
Kamati inayosimamia Ligi Kuu ya Ufaransa ina sheria kali zinazozuia klabu kubadilisha au kuongeza vitu vipya kwenye nembo rasmi ya klabu iliyosajiliwa kwa ajili ya msimu wa ligi.
Ripoti kutoka kwa wadau wa vifaa vya michezo zinaonesha kuwa PSG wataruhusiwa kutumia nembo hiyo yenye nyota mbili kwenye mashindano ya kimataifa tu, kama vile UEFA Champions League na Klabu Bingwa ya Dunia (FIFA Club World Cup).





