pmbet

Putin aahidi kuharibu ndege za kivita itakazopewa Ukraine

Eric Buyanza

March 28, 2024
Share :

Rais wa Urusi Vladimir Putin amezionya nchi za Magharibi kuhusu kuipatia Ukraine ndege za kivita aina ya F16 akisema hatua hiyo haitobadili chochote katika uwanja wa vita.
 

Putin amesema ndege hizo zina uwezo wa kubeba silaha za nyuklia na hilo atalizingatia katika mikakati ya kijeshi.
 

Putin alinukuliwa na mashirika ya habari ya Urusi akisema kwamba ndege hizo zitalengwa kokote zilipo na zitaharibiwa kama vifaa vingine.
 

Ubelgiji, Denmark, Norway na Uholanzi ni miongoni mwa nchi ambazo zimeahidi kutoa msaada wa ndege hizo za kivita za F-16 kwa Ukraine, huku muungano wa nchi nyingine ukiahidi kutoa mafunzo kwa marubani wa Ukraine wa namna ya kutumia ndege hizo. 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet