pmbet

Putin aamuru mazoezi ya silaha za nyuklia karibu na Ukraine

Eric Buyanza

May 7, 2024
Share :

Rais wa Urusi Vladimir Putin ameagiza kufanyika kwa mazoezi ya kijeshi yakihusisha silaha za nyuklia karibu na mpaka wa Ukraine. 

Kulingana na Rais Putin, hatua hiyo ni ya kushughulikia kile alichokiita ''kitisho'' cha nchi za Magharibi cha kupeleka vikosi vya Jumuiya ya kujihami NATO nchini Ukraine.

Wizara ya ulinzi ya Urusi haikutoa maelezo zaidi kuhusu tarehe ya kuanza kwa mazoezi hayo, lakini yatajumuisha vikosi vya wanaanga, majini na vile vilivyoko karibu na Ukraine.

Tangazo hilo limetolewa wakati vikosi vya Urusi vikidai kukamata vijiji viwili katika mikoa inayokabailiwa na vita ya Donetsk na Kharkiv mashariki mwa Ukraine.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet