pmbet

Putin aapa kujibu mashambulizi ya Ukraine

Eric Buyanza

March 16, 2024
Share :

Rais Vladimir Putin ameapa kujibu vikali msururu wa mashambulizi yaliyofanywa na Ukraine kwenye mpaka wa Urusi ambayo ameyataja kuwa ni jaribio la Kyiv la kuvuruga azma ya yeye kuchaguliwa tena.
 

Rais Putin alisema hayo alipolihutubia baraza lake la usalama katika siku ya kwanza ya uchaguzi unaofanyika kwa siku tatu ndani ya nchi hiyo na kwenye maeneo inayoyakalia kimabavu nchini Ukraine.
 

Putin ameahidi kujibu vikali mashambulizi hayo ya anga ya Ukraine kwenye maeneo ya mpakani ya Belgorod na Kursk yanayokabiliwa na mapigano makali katika siku za hivi karibuni.
 

Putin amekuwa madarakani tangu mwaka 1999 na anatazamiwa kubakia madarakani hadi 2030.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet