Putin aitolea masharti Ukraine ili amalize vita, Zelenskyy akataa
Eric Buyanza
June 15, 2024
Share :
Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema nchi yake itamaliza vita vyake dhidi ya Ukraine ikiwa nchi hiyo itakubali kuacha matarajio yake ya kujiunga na Jumuiya ya Kujihami ya NATO na kukabidhi majimbo manne inayoyadhibiti.
Hata hivyo Ukraine imeyakataa masharti hayo ya Urusi, huku mshauri wa rais wa Ukraine Mykhailo Podolyak akiyataja masharti hayo ya Putin ni sawa na kuiambia Ukraine ikubali kushindwa.