pmbet

Putin akutana na Xi Jinping China

Sisti Herman

November 18, 2026
Share :

 

Rais wa Urusi, Vladimir Putin, amewasili jijini Shenzhen nchini China kwa ajili ya kushiriki mkutano wa viongozi wa nchi za Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi ya Asia na Pasifiki (APEC), huku akitarajiwa kufanya mazungumzo ya pande mbili na Rais wa China, Xi Jinping.

Putin aliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Shenzhen Bao’an mapema Jumatano, Novemba 18, 2026, ambapo alipokelewa na Cai Qi, Mkuu wa Utumishi wa Rais Xi Jinping, katika mapokezi yaliyohudhuriwa pia na walinzi wa heshima wa jeshi la China.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Kremlin, mazungumzo ya viongozi hao yanatarajiwa kujikita katika kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi, hususan sekta za nishati, fedha, teknolojia na akili unde (AI), pamoja na masuala mbalimbali ya kimataifa.

Ziara hiyo inafanyika wakati ambapo ushirikiano wa kiuchumi na kimkakati kati ya Urusi na China ukiendelea kuimarika, huku biashara kati ya mataifa hayo ikifikia thamani ya rekodi ya dola bilioni 245 mwaka 2024.

Aidha, Putin anatarajiwa kushiriki mazungumzo ya pande tatu na Rais wa Marekani, Donald Trump, pamoja na Xi Jinping, yatakayofanyika Alhamisi, Novemba 19, pembezoni mwa mkutano wa APEC, ambapo masuala ya silaha za nyuklia na changamoto za usalama wa kimataifa yanatarajiwa kujadiliwa.

Mazungumzo hayo yanafuatiliwa kwa karibu kutokana na nafasi ya mataifa hayo matatu katika siasa za kimataifa, hususan katika kipindi ambacho dunia inakabiliwa na migogoro ya kijeshi na mvutano wa kisiasa.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet