Putin ampa zawadi ya gari Kim Jong Un
Eric Buyanza
February 20, 2024
Share :
Rais wa Urusi, Vladimir Putin amempa zawadi ya gari Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong Un.
Putin amemzawadia Kim Jong gari hilo la kifahari la Kirusi aina ya Aurus kama zawadi kwa sababu kiongozi huyo wa Korea Kaskazini alilipenda gari hilo alipoonyeshwa mwaka jana alipotembelea Urusi.
Gari hilo lililotengenezwa kwa ajili ya matumizi binafsi ya Kim lilikabidhiwa siku ya Jumapili, Shirika la Habari la Serikali la Korea (KCNA) limeripoti.
Dada yake Kim, Kim Yo Jong alimshukuru Putin kwa niaba ya kaka yake.
Kiongozi huyo wa Korea Kaskazini mara nyingi huonekana akiwa ndani ya gari aina ya Mercedes-Maybach Pullman Guard, yenye thamani ya zaidi ya dola milioni moja.