Putin ashambulia kijiji alichozaliwa Zelenskyy
Eric Buyanza
June 13, 2024
Share :
Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskyy, amesema shambulizi la anga la Russia, limepiga mji aliozaliwa wa Kryvyi Rih kusini mwa Ukraine siku ya Jumatano, na kuua takriban watu nane na wengine 21 kujeruhiwa.
Rais Zelenskyy alionyesha video ikimuonyesha mtu akiwa amebebwa kwenye machela na maafisa wa zimamoto huku moshi ukifuka kutoka kwenye majengo yaliyoharibiwa.