Putin ashinda kwa kishindo Urusi
Sisti Herman
March 18, 2024
Share :
Rais wa Urusi, Vladimir Putin ameshinda tena kwa kishindo na kuweka rekodi katika uchaguzi wa Urusi uliomalizika jana Jumapili, huku akiimarisha madaraka yake ambapo matokeo ya awali yanaonesha kuwa amepata asilimia 87.8 ya kura.
Akihutubia baada ya kumalizika kwa zoezi la upigaji Kura Putin amesema matokeo hayo yanapaswa kutuma ujumbe kwa Mataifa ya Magharibi kwamba Viongozi wake watalazimika kuitambua Urusi yenye ujasiri, iwe ni katika vita ama kwenye amani kwa miaka mingi ijayo.
Mitandao mbalimbali barani Ulaya imeripoti kwa kwa matokeo hayo yanayompa ushindi wa kishindo Putin mwenye umri wa miaka 71, anatazamiwa kuanza muhula mpya wa miaka sita utakaomfanya ampiku Josef Stalin na kuwa Kiongozi wa muda mrefu zaidi wa Urusi katika kipindi cha zaidi ya miaka 200 iwapo atamaliza muhula wake.
Putin amepata asilimia 87.8 ya kura, ikiwa hayo ni matokeo ya juu zaidi kuwahi kutokea katika historia ya Urusi baada ya muungano wa Kisovieti kuvunjika.
Mataifa ya Marekani, Ujerumani, Uingereza na mengine yamesema kuwa Uchaguzi huo haukuwa huru na haki kutokana na kufungwa kwa Wanasiasa wa upinzani na kudhibitiwa.