pmbet

Putin asitisha vita na Ukraine kupisha Pasaka ya Orthodox

Eric Buyanza

April 10, 2026
Share :

Rais wa Urusi Vladimir Putin ametangaza kusitisha mapigano kwa muda katika vita vya Ukraine ili kuadhimisha Pasaka ya madhehebu ya Orthodox.

 

Ikulu ya nchi hiyo ilisema katika taarifa jana Alhamisi kwamba usitishaji huo wa mapigano unatarajiwa kuanza Jumamosi saa kumi jioni na kudumu hadi Jumapili.

 

Hatua hiyo inakuja baada ya rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky kutoa wito mara kadhaa wa kusitisha mapigano wakati wa likizo. Wakristo wa Orthodox kama wale walio Urusi na Ukraine wanasherehekea Pasaka Aprili 12 mwaka huu.
 

Inaelezwa kuwa Waziri wa ulinzi Andrei Belousov aliamriwa kusimamisha shughuli zote za kijeshi kwa kipindi cha siku mbili za Pasaka.
 

Hata hivyo wanajeshi wameamuriwa kuwa tayari kujibu uchochezi wowote kutoka kwa adui.
 

DW

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet