pmbet

Putin atishia kutoa silaha kushambulia nchi za Magharibi

Eric Buyanza

June 6, 2024
Share :

Rais Vladimir Putin ameonya kwamba Urusi inaweza ikawapatia mataifa mengine makombora ya masafa marefu kwa ajili ya kushambulia nchi za magharibi. 

Putin aliyasema hayo alipokuwa akiongea na vyombo vya habari vya magharibi, na kusema itakuwa ni jibu kwao kutokana na ruhusa iliyotolewa na mataifa hayo kwa Ukraine kutumia silaha inazopewa na nchi hizo kuishambulia Urusi.
Putin pia amethibitisha kwa mara nyingine kuhusu utayari wa kutumia silaha za nyuklia ikiwa kutakuwa na kitisho chochote kwenye nchi yake.

Marekani na Ujerumani hivi karibuni waliiruhusu Ukraine kutumia makombora ya masafa marefu waliyoipatia kushambulia baadhi ya maeneo ndani ya Urusi.

"Kama mtu anadhani inawezekana kupeleka silaha kwenye uwanja wa vita ili kushambulia eneo letu na kutuletea matatizo, kwa nini na sisi hatuna haki ya kupeleka silaha kama hizo kwenye maeneo mengine duniani ambako wanaweza kushambulia maeneo muhimu kwenye mataifa ya magharibi?" alihoji Putin.

"Hilo litakuwa jibu linalowiana. Tutafikiria kuhusu hilo," aliwaambia waandishi hao wa habari, huku akipuuzilia mbali madai kwamba Urusi inapanga kuwashambulia wanachama wa NATO.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet