Pyramid kama la Misri lajengwa USA
Sisti Herman
July 3, 2025
Share :
Piramidi kubwa kama zile za kale zinazopatikana Misri limejengwa huko Tennessee nchini Marekani.
Piramidi ya Memphis huko Tennessee ina urefu wa futi 321, na kuifanya kuwa moja ya piramidi kubwa zaidi Duniani.
Hapo awali ilijengwa kama uwanja wa michezo, lakini sasa ni nyumbani kwa duka kubwa la Bass Pro Shops, hoteli, mikahawa, na hata bwawa la ndani.
Inashikilia rekodi ya ulimwengu kwa jengo kubwa zaidi la kibiashara lenye umbo la piramidi.